Wednesday, 23 March 2016

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA AFICHUA MPANGO WA KUMNG'OA MADARAKANI


MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Dk Jesca Msambatavangu amefichua mpango wa kumng’oa madarakani aliosema unaratibiwa na wajumbe wawili wa kamati ya siasa ya mkoa huo pamoja na aliyewahi kuwa waziri katika awamu moja ya serikali zilizopita.

Akizungumza na wanahabari jana Dk Msambatavangu aliyeapa kupigania haki yake ndani ya chama hicho hadi tone la mwisho la jasho lake alisema wajumbe hao wanaratibu mpango huo kwa kutumia baadhi ya vijana wa chama hicho kutoka wilaya zote tatu za mkoa wa Iringa za Mufindi, Kilolo na Iringa.

“Toka Machi 19 hadi juzi Machi 23 vijana hao walikutanishwa katika eneo la Ilala, mjini Iringa na kupanga na kupeana majukumu ya namna watakavyotekeleza mpango huo,” alisema bila kutaja majina ya waratibu na vijana hao zaidi ya 10.


Alisema juzi alifanikiwa kupata siri za kikao hicho kutoka kwa baadhi ya vijana hao ambao hawakuridhishwa na gharama wanayotakiwa kulipwa kwa ajili ya kuufanikisha mpango huo walioubatiza jina la “oparesheni kumng’oa Jesca madarakani.”

Kwa taarifa zaidi soma gazeti la Habarileo la Machi 25

Reactions:

0 comments:

Post a Comment