Wednesday, 2 March 2016

MTOTO WA RAILA ODINGA AWAOMBA RADHI WATANZANIA

Untitled

Mtoto wa aliyekuwa Waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary Odinga, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya wakati liko Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rosemary amesema nia yake ilikuwa ni kusema kuwa alipokuwa shuleni alifundishwa kuwa fuvu la mtu wa kale Olorgesaiile lipo eneo la Kajiado.

“Bonde la Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York, Marekani (International Young Leaders Assembly). Nawaombeni radhi Watanzania.

Olduvai Gorge iko salama wala haijanyakuliwa na Kenya, katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu cha ubinadamu” alisema Bi. Odinga.


Mwishoni mwa wiki iliyopita kulizagaa vipande vya video vikimuonesha binti huyo akihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani na kusema bonde la Olduvai gorge lipo nchini Kenya.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment