Wednesday, 9 March 2016

MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII KUWAGHARIMU WATUMISHI

150115131948_whatsapp_640x360_getty_nocredit

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbalawa, amepiga marufuku wafanyakazi ndani ya Wizara hiyo kutumia simu na kuchati kwenye mitandao ya kijamii wawapo ofisini humo.

Akizungumza katika kikao na wafanyakazi wote, katika ukumbi wa Karemjee Mbalawa amedai asiyefata maagizo hayo atatumbuliwa jipu bila huruma.

“Kuna tabia ya wafanyakazi kuwasili ofisini hadi saa nane mchana, kisha wanazama kwenye porojo na kutumia muda mwingi katika mitandao ya jamii na matokeo yake muda wa kazi unaisha wakiwa hawajafanya lolote kiuzalishaji. Tabia hii ikome mara moja,” alisema Profesa Mbarawa.


Amewataka watumishi hao kuzingatia weledi, dhima na kazi kwa bidii kwa manufaa ya Taifa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment