Sunday, 13 March 2016

MAKONDA AMNG'0A MECK SADICK DAR ES SALAAM, MASENZA NGANGARI IRINGA

Bw. Paul Makonda (kushoto) pamoja na Bw. Mek Sadick.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Paul Makonda leo ameteuliwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuwa mkuu wa  Mkoa wa Dar es salaam  na kumuhamisha  Said Meck Sadick  kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.

Aidha, Makonda hivi karibuni amejizolea umaarufu kufuatia kufanikiwa kuwasafirisha walimu bure kwenye daladala mpango ulioanza wiki iliyopita licha ya kukumbwa na Changamoto kadhaa ikiwemo walimu kubughuziwa na makondakta.

Licha ya kuwasafirisha walimu bure Makonda amekuja wazo jipya lingine  lijulikanalo kama mtaa wa baa kufuatia Wilaya ya Kinondoni kugubikwa na baa  katika maeneo  mengi  ikiwemo jirani na misikiti na  Makanisa.

Mpango huo ni maalumu kwa ajili za kuweka baa zote sehemu moja ili kuepusha bughuza kwa watu wengine wasiojihusisha na starehe mbalimbali zinazopatikana kwenye baa hizo.

Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wakihamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

Akitangaza uteuzi huo, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe Ikulu Jijini Dar es Salaam, amesema Wakuu wa Mikoa walioteuliwa na Rais ni kama ifuatavyo.

Mh. Paul Makonda (Dar es Salaam), Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga (Geita), Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu (Kagera), Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga (Katavi), Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (Kigoma), Mh. Godfrey Zambi (Lindi), Dkt. Steven Kebwe (Morogoro), Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven (Rukwa), Mh. Anna Malecela Kilango (Shinyanga), Mhandisi Methew Mtigumwe (Singida), Mh. Antony Mataka (Simiyu), Mh. Aggrey Mwanri (Tabora), Mh. Martine Shigela (Tanga), Mh. Jordan Mungire Rugimbana (Dodoma), Mh. Said Meck Sadiki (Kilimanjaro), Mh. Magesa Mulongo (Mara), Mh. Amos Gabriel Makalla (Mbeya).

Wengine ni Mh. John Vianey Mongella (Mwanza), Mh. Daudi Felix Ntibenda (Arusha), Mh. Amina Juma Masenza (Iringa), Mh. Joel Nkaya Bendera (Manyara), Mh. Halima Omary Dendegu (Mtwara), Dkt. Rehema Nchimbi (Njombe), Mhandisi Evarist Ndikilo (Pwani), Mh. Said Thabit Mwambungu (Ruvuma) na Luteni Mstaafu Chiku Galawa (Mkoa Mpya wa Songwe).

Reactions:

0 comments:

Post a Comment