Tuesday, 15 March 2016

MAGUFULI AAPISHA WAKUU WA MIKOA WAPYA AKIWATAKA WAWASHUGHULIKIE WAFANYAKAZI HEWA

15

Rais Dk John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa mikoa wapya aliowaapisha leo Ikulu jijini Dar es Salaam kuhakikisha majina ya watumishi hewa waliopo katika halmashauri na idara za serikali mikoani yanaondolewa ndani ya siku kumi na tano.

Amesema tatizo la wafanyakazi hewa limekuwa likigharimu serikali fedha nyingi, ambapo ametolea mfano wa uchunguzi uliofanywa katika mikoa miwili ya Dodoma na singida na kubaini takriban wafanyakazi hewa 202 katika halmashauri 14.

Amesema kutokana na hali hiyo na ikichukuliwa taswira ya nchi zima, hasara inayotokana na malipo ya mishahara hewa inaweza kufikia zaidi ya shilingi billioni mbili, hivyo amewataka kuzisimamia vyema halmashauri.

Rais Dk Magufuli amesema hayo mara baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amewahimiza kuhakikisha wanatatua kero za wananchi, na kudumisha usalama wa raia  wakiwa ndiyo mwenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama katika mkoa husika, pamoja na kuhakikisha vijana wanafanya kazi katika mikoa yao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment