Monday, 21 March 2016

DK SHEIN ASHINDA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amemtangaza  Mgombea wa urais kupitia chama cha CCM Visiwani Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuwa ndiye mshindi wa  kiti cha urais baada ya kupata kura 299,982 sawa na asilimia 91.4 ya kura zote halali 328,327 zilizopigwa.

Dr. Shein ameshinda urais katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana baada ya ule wa awali kufutwa Oktoba 25 kwa madai ya  ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi huo.


Mbali na Dr. Shein kushinda,vyama vya upinzani takribani 10 vilitangaza kususia uchaguzi huo kikiwemo chama kikubwa cha Upinzani cha CUF.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment