Sunday, 6 March 2016

DK MAGUFULI AMNG'OA BALOZI SEFUE, ATEUA MWINGINE


RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Balozi Ombeni Sefue.

Kabla ya Uteuzi huo, Kijazi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi wakati huo Dk Magufuli akiwa waziri wake. Baada ya kuondolewa katika nafasi hiyo Balozi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Taarifa ya Ikulu imesema baada ya uteuzi huo mpya, Balozi Sefue atapangiwa kazi nyingine.


Swali lililobaki ni kazi gani atapangiwa Balozi Sefue yenye hadhi sawa na Katibu Mkuu Kiongozi?

Reactions:

0 comments:

Post a Comment