Sunday, 13 March 2016

DARAJA LA MTO KILOMBERO KUKAMILIKA NOVEMBA MWAKA HUU

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeupe) akishuka kutoka katika kivuko cha Mv Kilombero mara baada ya kukagua utendaji kazi wa Nahodha wa kivuko hicho.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha ujenzi wa daraja la mto Kilombero unakamilika ifikapo Novemba, mwaka huu ili kumaliza changamoto ya usafiri inayowakabili wananchi wa wilaya za Kilombero na Ulanga mkoani Morogoro.

Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo Wilayani Kilombero mara baada ya kukagua maendeleo ya kivuko cha Mv- Kilombero kilochokuwa kinakarabatiwa kufuatia kuzama mwishoni mwa mwezi Januari.

Amesema tayari mkandarasi anayejenga daraja hilo kutoka China ameshalipwa shilingi bilioni 11.2 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambapo hivi sasa kazi inayoendelea kwa mkandarasi huyo ni kutengeneza vifaa maalumu kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo huko nchini China

Reactions:

0 comments:

Post a Comment