Wednesday, 9 March 2016

AJALI YAUA WANNE, WENGINE 25 WAJERUHIWA


WATU wanne wamethibitishwa kufa baada ya kutokea ajali mbaya maeneo ya Al hamza jirani na daraja la Tabata Matumbi.

Miongoni mwa  waliokufa ni Godfrey Nyawenga na wengine watatu bado kutambuliwa.

Aidha majeruhi  25 akiwamo mtoto wa mwaka mmoja walipatikana na watu watano wako katika hali mbaya na wamekimbizwa Muhimbili kutoka hospitali ya amana akiwamo mtoto wa mwaka mmoja.


Ajali hiyo mbaya  kabisa ilihusisha magari matatu likiwemo Dalalada ya abiria linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto kwenda Ubungo,  lori la mchanga na lori la ng’ombe. 

Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugonga na Lori lingine lililokuwa limebeba ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment