Monday, 22 February 2016

WAZIRI KAIRUKI ATUMBUA JIPU BILA GANZI


WAZIRI  wa nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi  na Utawala Bora, Angella Kairuki amemsimisha kazi Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, (TPSC), Said Nassoro kuanzia leo Februari 22, 2016.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2016, Waziri huyo alisema, Mkuu huyo wa Chuo amesimamishwa kazi kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo na kuisababishia serikali kupata hasara ya Shilingi Bilioni 1.

 Wengine waliokumbwa na “fagio” la leo ni pamoja na Mkuu wa Chuo hicho tawi la Dar es salaam, Joseph  Mbwilo na Mkuu wa Chuo hicho tawi laTabora, Silvanus  Ngata. Waziri baada ya kubaini kuwepo na utendaji usio ridhisha katika vyuo hivyo, ameona hakuna budi bali kuchukua uamuzi huo.

Amesema Nassoro amemsimisha kazi baada ya kushindwa kuwasimamia watumishi wa chini yake katika  chuo hicho na pia kuwa na usimamizi usio na ufanisi.

 “Mwaka  2011 hadi  2013 Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la chuo cha Mtwara tofauti na ile fedha iliyopangwa, na hata ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali ilithitisha ubadilifu huo,” alisema.

Pia waziri Kairuki amesema amemsimamisha Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za chuo, Waziri Kairuki alitoa tamko hilo mbele ya bosi huyo wa Chuo Cha Utumishi Nasoro ambaye alikuwa meza moja naye.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment