Friday, 19 February 2016

WANAWAKE WA CUF KUFANYA MAANDAMANO KUPINGA HALI YA KISIASA ZANZIBAR

Mwenyekiti wa  jumuiya Wanawake CUF Severena Mwijage.

Jumuiya ya  Wanawake ya Chama cha Wananchi (JUKECUF) inatarajia kufanya maandamano ya amani Februari  22, mwaka huu jijini Dar es salaam ikilenga kupinga hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Severena Mwijage amesema kwamba maandamano hayo yataanzia ofisi kuu za CUF buguruni kuelekea ofisi ya makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu.

Amesema Maandamano hayo yatapita barabara ya uhuru, ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam, Karume, Kariakoo, Mnazi mmoja, Central polisi, barabara ya Sokoine , Bandarini, Mahakama kuu, Mahakama ya ardhi hadi ofisi ya makamu wa Rais.

Ameongeza  kuwa jumuiya hiyo inatambua kwamba hali ya Amani iliyopo Zanzibar ikivurugika kwa kiasi kikubwa watakaoathirika ni akina mama na watoto hivyo wameona  ni bora kufikisha kilo chao kwa makamu wa Rais ambaye ni mwanamke mwenzao ili awasaidie.


Hata hivyo maandamano hayo hayapewa kibali na Jeshi la Polisi, hivyo huenda wakaruhusiwa au wasiruhusiwe kutokana na Rais aliyepo Madarakani kupiga marufuku maandamano ya kisiasa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment