Sunday, 21 February 2016

WALIOTAKA BINADAMU WARUHUSIWE KUJAMIIANA NA WANYAMA WASHINDWA KESI


JUHUDI za wajerumani wawili kutaka katiba ya nchi hiyo kubadilishwa ili kuruhusu binadamu kufanya mapenzi na wanyama zimeshindwa baada ya mahakama ya katiba ya nchi hiyo kusema ‘NO’.

Watu hao wawili waliotaka Mahakama ya katiba kubadili sheria wamesema kwamba wao wanapenda kufanya mapenzi na wanyama.

Ujerumani ina sheria kali kuhusiana na tendo la kufanya mapenzi na wanyama.
Wawili hao ambao majina yao hayakutamkwa walipeleka shauri lao Karlsruhe wakitaka wafikiria na kutoa maamuyzi kwamba sheria zilizopo sasa zinazozuia mapenzi na wanyama zinakwenda kinyume na katiba.

Mahakama hiyo ilisema kwamba zuio hilo haliendi kinyume na katiba na linakubalika..

Mahakama hiyo ilisema kwamba kitenndocha kuwepo kw asheria ya kuzui ngono ya binadamu na wanyama ni kitendo chema kuzuia wanyama kunyanyasika na mashambulio ya ngono na wakware.


Sheria ya kulinda wanyama ya Ujerumani inasema wazi kwamba wanaolazimisha wanyama kushiriki katika ngono na watu watalipa faini ya euro 25,000 ( sawa na dola 27,700; au paundi 19,000) 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment