Wednesday, 10 February 2016

VYAMA TISA VYAJITOA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR


VYAMA tisa vya siasa kati ya 14 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu Zanzibar mwaka jana vimeungana na chama cha wananchi (CUF)  kutoshiriki uchaguzi wa marudio unaotegemewa kufanyika Machi 20 mwaka huu.

Mratibu wa vyama hivyo, Kassim Bakari alisema vyama hivyo viliazimia kutoshiriki uchaguzi huo baada ya kukutana kwenye mkutano wa pamoja Unguja.

Vyama hivyo ni UMD, Jahazi Asilia, Chaumma, UPDP, DP, CCK, ACT Wazalendo.

Hata hivyo alisema ushiriki wa ADC na CCK bado una utata kwani mapema wiki iliyopita wagombea wake walitangaza kushiriki licha ya vyama vyao kutokubaliana nao hali iliyopelekea wagombea hao  kusimamishwa uanachama wa vyama wanavyotoka.


Vyama vilivyotangaza kurudia uchaguzi hadi sasa ni CCM, Tadea, TLP, Sau na AFP.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment