Wednesday, 3 February 2016

TIGO YAWAPA WATEJA WAKE HUDUMA YA WHATSAPP BURE


Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma hiyo  ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu  kutoa ofa ya bure  ya mtandao huo wa jamii  nchini.

 Akitangaza upatikanaji bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habarijijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja wote wa Tigo  wanaotumia  vifurushi vya intaneti  vya kampuni hiyo kwa wiki na mwezi  watapata huduma ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.

Huduma ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma ujumbe  kwa njia ya simu, ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania  na  duniani  inatumiwa na watu wapatao milioni 900. WhatsApp inawezesha watumiaji  kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.

“Kuanzia sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua vifurushi vyetu vya wiki au mwezi  watakuwa na fursa ya kufurahia  WhatsApp BURE. Hili linawezekana kama mteja ana smartphone. Huduma ya bure ya WhatsApp kwa wateja wetu inaonesha  jinsi tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko kwenye  maisha ya kidijitali  na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.

Kwa Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo analohitaji mteja wa Tigo ni kuwa na  kifurushi cha intaneti  cha wiki au mwezi  ambacho anaweza kukipata kupitia *148*00# √É Tigo-Tigo Xtreme/MiniKabang√É  Wiki au Mwezi + WHATSAPP YA BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki simu  za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60.

WhatsApp ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma ya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment