Tuesday, 2 February 2016

SITA WANASWA WAKIHUSISHWA KUTUNGUA HELIKOPTA YA DORIA

ndege iliotunguliwa

JESHI la Polisi linawashikilia watu sita wanaodaiwa kuwa majangili, wakituhumiwa kuitungua helikopta ya doria na kusababisha kifo cha rubani wake katika pori la akiba la Maswa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushy amethibitisha kukamatwa kwa watu hao na kusema watuhumiwa hao walikamatwa juzi na wanalisaidia jeshi hilo katika uchunguzi wake.

Ijumaa iliyopita, watu wasiojulikana, waliitungua helikopta hiyo  wakati ikifanya doria katika pori hilo baada ya kuwapo taarifa kwamba kuna tembo watatu wameuawa na majangili katika pori hilo.


Katika tukio hilo, rubani wa helikopta hiyo raia wa Uingereza, Rodgers Gower (37) alikufa, huku mwenzake Nicky Bester wa Afrika Kusini akinusurika.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment