Sunday, 7 February 2016

POLISI WATATU WAFARIKI KWENYE MSAFARA WA DK MAGUFULI


Jeshi la Polisi mkoani Singida limepoteza Askari 3 waliofariki dunia baada ya gari lao lililokuwa kwenye msafara wa Rais John Magufuli kutoka Singida kwenda Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka alisema ajali hiyo ilitokea saa 9.40 alasiri, katika Kijiji cha Isuna, Wilaya ya Ikungi mkoani humo baada ya moja ya matairi ya gari hilo kupasuka na dereva kushindwa kulimudu.

Gari hilo lililopata ajali ni lile lililokuwa limetangulia ili kufagia barabara kabla ya msafara wa Rais, likiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha mkoa huo.

ACP Thobias  aliwataja waliofariki kuwa ni Mkaguzi Mwajelo, Sajenti Elias Mrope na Sajenti Gerard.

Waliojeruhiwa ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Singida (RCO), Peter Majira (50 na PC Charles Simon (34) ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Rais Magufuli alikuwa mjini Singida alikokuwa amekwenda kushiriki maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment