Tuesday, 23 February 2016

POLISI DAR WAKUSANYA BILIONI 1.9 ZA MAKOSA YA BARABARANI

siro

Kikosi cha usalama barabarani kanda ya Dar es Salaam kimekusanya zaidi ya Sh bilioni 1.9 kama faini za makosa ya barabarani kati ya Februari 1 na 22, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema madereva wengi hawafuati sheria za usalama barabarani hivyo kuwalazimu askari kuwatoza faini hizo.


Kwa sasa askari wa usalama barabarani hutumia mashine za kielectroniki  (EFD) jambo linalopelekea ukusanyaji mzuri wa mapato.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment