Saturday, 27 February 2016

OMBA OMBA ANAYETUMIA KISU KULAZIMISHA MISAADA AKAMATWA MJINI IRINGA


YULE omba omba maarufu wa mjini Iringa, Mohamed Chengulla anayetumia kisu kuwatisha watu anaotaka wamsaidie fedha amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa  wa Iringa baada ya msako mkali kufanywa dhidi  yake.

Kijana huyo alikamatwa leo leo majira ya saa 5 asubuhi katika eneo la Posta  mjini Iringa baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa  wananchi, hasa  wanawake ambao  wamedai kufukuzwa mara kwa mara na kijana huyo akiwa na kisu chake mkononi baada ya kunyimwa pesa anazotaka kusaidiwa.


Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba pamoja na kuthibitisha  kutokea kwa  tukio hilo ametaka wananchi  kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo pindi wanapoona au kukutana na matukio yanayohatarisha usalama wa mali na maisha yao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment