Sunday, 28 February 2016

NDALICHAKO ATUMBUA MAJIPU MATATU TAASISI YA ELIMU

Watumishi watatu wa Bodi ya Taasisi ya Elimu nchini (TET)  wamesimamishwa  kazi  kwa kushindwa kusimamia   sheria ya manunuzi na kazi ya uchapaji wa vitabu.

Hayo yamebinishwa na Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ambapo amewataja  waliosimamishwa  kazi kuwa ni  Peter Bandio, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Vifaa vya Kielimu, Pili Magongo Mwanasheria wa TET na Jackson Mwaigonela Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi.

Amesema   watumishi hao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuruhusu vitabu hivyo kuchapishwa vikiwa na mapungufu.

“Mnamo tarehe 22 Januari mwaka 2016 bodi hiyo ilishauriwa kusitisha uchapaji wa vitabu uliokuwa ukifanywa na kampuni ya Yukos Enterprises Ltd baada ya kubainika kuwa na mapungufu, lakini haikusitisha,” ameongeza.

Amesema  kuwa  Serikali iliamua kusitisha uchapishaji wa vitabu hivyo ili isiendelee kupokea vitabu vyenye mapungufu, hata hivyo taasisi ya elimu haikusitisha uchapishaji wa vitabu hivyo, badala yake kampuni hiyo ilichapisha vitabu vyote ilivyopangiwa.

Kutokana na mapungufu hayo, Wizara imetoa maagizo ya kuondolewa kwa baadhi ya vitabu vilivyowasilishwa kwenye bohari ya serikali ifikapo tarehe 29 Februari mwaka huu.

Kwa upande wa  Mapungufu yaliyoonekana kwenye vitabu hivyo ni  upungufu wa mwingiliano wa rangi, upungufu wa kurasa katika vitabu, ukataji usiozingatia vipimo,vitabu kuchakaa kabla ya matumizi na mpangilo mbaya wa kurasa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment