Friday, 12 February 2016

NCHEMBA ALIVYOWANASA WEZI WA USHURU MACHINJIO YA UKONGA

Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba akizungumza katika machinjio ya Ukonga.

Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba amewafukuza kazi viongozi wote wa Machinjio ya Ukonga Mazizi kufuatia   kuiibia serikali fedha za ushuru wa kuchinjia ng’ombe.

Nchemba aliyefanya ziara ya kushitukiza usiku wa kuamkia leo amekamata ng’ombe 200 wakiwa wanaingizwa kwenye machinjio bila kibali halali, na kati yao ni ng’ombe 20 tu ndo walikuwa na kibali cha kuchinjwa, hivyo ushuru  wa ng’ombe180  ulikuwa  unatafunwa  na  viongozi wa machinjio hayo.

Kufuatia kubaini wizi huo wa fedha za umma Nchemba ameagiza  vyombo  vya  dola  viwakamate  viongozi  wote waliohusika katika machinjio hiyo na  kuwafikisha  mahakamani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment