Sunday, 21 February 2016

MPANGO WA KUSITISHA MATUMIZI YA SIMU FEKI WAWALIZA WAFANYABISHARA NA WATUMIAJI

Baadhi ya simu za kisasa (smart Phones).

Mpango wa serikali kuzima simu feki Juni 17, mwaka huu umeanza kuwaliza wafanyabiashara wengi wa simu hizo katika maeneo mbalimbali nchini wanaolalamika kukosa wateja.

Baadhi ya Wafanyabishara hao wameeleza kuwa na mzigo mkubwa wa simu hizo katika maduka yao.

Hivi karibuni mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) ilitangaza kuzima simu zote feki ifikapo tarehe hiyo kwa maelezo kwamba simu hizo zina madhara kwa watumiaji.


Wakati wafanyabiashara wakilalamika kupata hasara, upande wa watuamiaji nao wamelalamika kuwa watakosa mawasiliano kwa kuwa uwezo wao wa kununua simu origino zinazouzwa kwa bei kubwa ni mdogo.

Wakizungumzia mpango wa kuzimwa kwa simu hizo, wafanyabiashara hao wameiomba serikali iongeze muda ili waweze kupunguza hasara kwa kuziuza hata kwa bei pungufu zaidi.

“Ndio waongeze muda ili tueze na wanunuzi wapate muda wa kutumia,” alisema mfanyabishara mmoja wapo bila kuelezea madhara kwa watumiaji.

Nao watumiaji wameilaumu serikali kutoa agizo la kuzimwa kwa simu feki huku ikiruhusu simu hizo kuingia nchini.


Zoezi la kufungiwa kwa simu feki sio geni kwa nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya ambao tayari wameshazifungia kabisa simu hizo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment