Monday, 29 February 2016

MOTO WATEKETEZA BWENI LA WAVULANA IYUNGA SEKONDARI

moto 1

MOTO mkubwa umeteketeza bweni la wavulana katika shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya huku chanzo cha ajali hiyo kikielezwa kuwa ni hitilafu ya umeme.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyirembe Munasa amesema moto huo umetokea leo majira ya saa tatu asubuhi wakati wanafunzi wanaotumia bweni hilo wakiwa madarasani.

Munasa amesema kwa kushirikiana na kikosi cha Zima moto pamoja na kamati ya ulinzi na usalama waliuzima moto huo mapema na kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine.


Bweni lililoungua lilikua linahifadhi wanafunzi 95. Baadhi ya wanafunzi wamefanikiwa kuokoa vifaa vyao kwa masaada wa watu wa zimamoto.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment