Friday, 19 February 2016

MCHINA ASHIKA NAMBA MBILI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015

 Congcong Wang (Kulia) aliyeshika nafasi ya pili kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha nne hapa Tanzania yaliyotoka jana akiwa na mama yake mzazi

WAKATI Kiswahili kikiendelea kuleta shida kwa wanafunzi wengi wa kitanzania,  binti mwenye asili ya kichina Congcong Wang (Kulia kwenye picha juu) mbali na kushika nafasi ya pili kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa jana, alipata alama B katika mtihani huo wa Kiswahili.

Binti huyo alikuwa anasoma shule ya sekondari ya wasichana ya Feza (Feza Girls) iliyopo jijini Dar es Salaam.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment