Sunday, 28 February 2016

KIKWETE KUONGOZA KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA WA KIFO CHA KOMBA

2dfgbb

Familia ya marehemu, John Komba inatarajia kuzindua kitabu cha historia yake leo kuanzia alipozaliwa hadi alipofikwa na umauti ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu alipoitwa mbele ya haki.

Kumbukumbu ya mwaka mmoja ya marehemu John Komba aliyekuwa Mbunge wa Mbinga itaongozwa na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete nyumbani kwa familia ya marehemu.

Mjane wa marehemu Salome Komba amesema wazo la kumbukumbuku hiyo limetolewa na wanafunzi ambao walishawahi kufundishwa na marehemu kwa kushirikiana na familia.

“Kumbukumbu ya marehemu mume wangu imeandaliwa na wanafunzi ambao aliwafundisha Komba na mimi na mgeni rasmi katika shughuli hii anatarajia kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete,”alisema Mama Salome.

Ameongeza kuwa uzinduzi wa kitabu hicho na kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo chake utahudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya upinzani watahudhuria.

Salome alisema kitabu hicho kiliandikwa na Komba mwaka 2002 lakini hakufanikiwa kukitoa hivyo wao kama familia wameamua kuendeleza pale alipoishia kuandika na kumalizia na kukizindua leo.

Salome ni Mwalimu wa Hesabu na Kiingereza na aliwahi kufundisha shule ya msingi Wilolesi iliyopo Iringa mwaka 1978 na 1979 hadi 1997 alifundisha shule ya Lugalo na Kawe za Dar es Salaam.

Alisema pia wanafunzi walisomeshwa na Komba pamoja na yeye wanatarajia kufanya harambee kwa ajili ya kuanzisha shule ya kumbukumu ya Komba.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment