Saturday, 27 February 2016

KAMPUNI YAJENGA KITUO CHA UCHANGIAJI DAMU IRINGAKAMPUNI ya Asas Group yenye makao yake makuu mjini Iringa, imejenga kituo cha kisasa cha uchangiaji  wa damu ndani ya hospitali ya mkoa wa Iringa ili kuboresha huduma hiyo.

Kituo hicho ambacho haikuelezwa kimejengwa kimeanza kutoa huduma hiyo hivikaribuni ikiwa ni pamoja na kupokea wasamalia wema wanaotaka kutunisha benki ya damu ambayo mahitaji yake ni makubwa yakiongezeka siku hadi siku.

Mkuu wa  Kitengo  cha Damu  Salama Mkoa wa Iringa,  Hubert Swallo amesema idadi kubwa ya watu wanajiotokeza kuchangia benki hiyo ya damu ni wale ambao ndugu zao wanahitaji huduma hiyo.

“Ombi letu ni kwa wananchi bila kujali wana wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu au hawana wajitokeze kuchangia damu katika benki hii, ili ituwezeshe kuwa na akiba ya kutosha kulingana na mahitaji,” alisema.

uthibitishia mtandao huu  kuwepo kwa changamoto  kubwa ya  wananchi  kufika kwa ajili ya  kujitolea  damu pasipo  kuombwa na jamaa  zao.

Swallo  alitoa  wito kwa taasisi  zikiwemo za  dini, vyuo na shule  mbali mbali  kujitokeza  kuchangia damu.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment