Sunday, 21 February 2016

JEB BUSH AJITOA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS MAREKANI, BILIONEA TRUMP AZIDI KUPETA


Gavana wa zamani wa Florida Jeb Bush amejiondoa katika kinyang’anyiro cha kutafuta kuwani kugombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.

Amejiondoa baada ya kutofanya vyema katika uchaguzi wa mchujo majimbo matatu ya kwanza ya Iowa, New Hampshire na South Carolina.

Katika mchujo wa South Carolina jana, Jeb Bush alishika nafasi ya nne huku ushindi wa kwanza ukienda kwa Bilionea Donald Trump aliyepata zaidia ya asilimia 32 ya kura za wa republican.

“Leo nasitisha kampeni yangu,” Bwana Bush aliyepigiwa upatu wa kufanya vyema katika harakati zake hizo aliwaambia wafuasi wake.

Jeb Bush ni kakake rais wa zamani George W Bush na mwanawe Rais wa zamani George H W Bush.

Katika jimbo la South Carolina, ambapo alitarajia sana kufufua kampeni yake, alimaliza wa nne akishikilia nafasi hiyo pamoja na gavana wa Ohio John Kasich.

“Watu wa Iowa, South Carolina na New Hampshire wamenena, na naheshimu uamuzi wao,” gavana huyo wa zamani amesema, akirejelea kutofana kwake katika majimbo hayo matatu ambayo yamefanya uchaguzi wa mchujo.

“Nimekuwa na maisha mazuri na kwangu kutumikia umma limekuwa jambo kuu zaidi katika maisha yangu haya,” alisema.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment