Wednesday, 3 February 2016

HUU NDIO USAFIRI BINAFSI WA TRUMP KATIKA KAMPENI ZAKE ZA URAIS MAREKANI, UNA THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 157
SEMA chochote unachoweza kusema kuhusu mgombea anayetafuta kuwania urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump; jamaa anajua kufanya safiri kwa mbwembwe za aina yake.

Jumamosi iliyopita, wafuasi wake wa Iowa waliojionea bilionea huyo akishuka na ndege yake kubwa ya kifahari, Trump Force One inayofananishwa na ndege inayotumiwa na Rais wa Marekani, Air Force One.

 Taarifa iliyochapishwa na New York Times, inasema baada ya kununuliwa na Trump ndege hiyo yenye thamani ya zaidi ya Pauni za Kingereza Milioni 63 (Zaidi ya Sh Bilioni 157 ) ilinakshiwa kwa dhahabu katika maeneo yake mengi.

Jambo la ziada katika ndege hiyo aina ya Boeing 757 ni kwamba ina viti 43, wakati uwezo wake ni kuwa na viti 180 hadi 200 kutokana na ukubwa wake.

Ikiwa na vyumba vya ziada, ndege hiyo imegawanywa katika maeneo muhimu kama chumba cha chakula, chumba cha VIP na eneo la kupumzikia lenye televisheni yenye ukubwa wa Inchi 57.

Na kama hutaki kuangalia TV ya pamoja, kila kiti kimeunganishwa na TV yake ambayo unaweza kuitumia kungalia program unayotaka.

Ndege hiyo pia ina chumba maalumu cha kulala Trump ambacho kina kitanda cha saizi ya malkia, na ambacho pia kimenakshiwa kwa dhahabu katika kuta zake.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment