Sunday, 21 February 2016

DK BESIGYE APINGA MATOKEO YA URAIS UGANDA

Dkt. Kizza Besigye

Mmoja wa wapinzani wakuu katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni  nchini Uganda, Dk Kizza Besigye, amekatalia mbali matokeo ya uchaguzi huo, uliofanyika siku ya Alhamisi.

Dk Besigye ambaye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu Ijumaa amesema raia nchini Uganda wameshuhudia ulaghai mkubwa katika uchaguzi mkuu wa taifa hilo la Mashariki mwa Afrika.

Kanali huyo mstaafu ameelezea uchaguzi huo kwamba sio hali na akaufananisha na mapinduzi ya kijeshi.

Rais Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 30 sasa, alipata zaidi ya asilimia 61 ya kura huku Besigye akijipatia asilimia 35 ya kura.


Wachunguzi wa kimataifa wanasema kuwa uchaguzi huo uliandaliwa katika mazingara ya hofu na kudhalalishwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment