Monday, 1 February 2016

BUNGE LAKAA KAMA KAMATI KUJADILI MPANGO WA MAENDELEO


Hatimaye Bunge limeanza kujadili mpango wa maendeleo wa mwaka 2016/2017 kama kamati leo baada ya kutengua kanuni ya 94 (1) ili wabunge waweze kujadili, kushauri na kuuboresha mpango huo kabla ya kufikishwa katika bunge la bajeti baadaye mwaka huu.

Mpango huo uliingia dosari wiki iliyopita baada ya wabunge wa upinzani kukataa kuujadili kwa madai kuwa serikali ilikiuka kanuni na taratibu za kuuwasilisha bungeni.

Akiwasilisha Mpango huo Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema mpango huo umeweka kipaumbe cha kuanzisha na kuendeleza viwanda vinavyotokana na rasilimali zinazopatikana nchini pamoja na viwanda vya kuzalisha bidhaa zinazotumiwa na watu wengi.

Dk Mpango amesema katika mapango huo serikali imepanga kukusanya shilingi trilioni 14.16 kutokana na mapato ya kodi ambayo ni ongezeko la asilimia 15 ikilinganishwa na mapato ya kodi ya fedha yaliyokusanywa mwaka uliopita.

Aidha katika mwaka wa fedha 2016/2017, serikali imepanga kutumia shilingi trilioni 22 .99 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo ambapo kati ya hizo trilioni 16.80 itakuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 6.18 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Amesema kati ya trilion 16.80 za matumizi ya kawaida, shilingi trilion 6.65 zitakuwa ni kwa ajili ya mishahara.

Aidha amesema kuwa kati ya trilion 6.18 za miradi ya maendeleo, takriban trilion 4 sawa na asilimia 77.8 zitakuwa ni fedha za ndani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment