Tuesday, 23 February 2016

AJALI YAUA WATU WANNE MKOANI MARA

ajali 2

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa baada ya basi waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kugonga nguzo na kupinduka mkoani Mara.

Ajali hiyo iliyohusisha basi aina ya Scania lenye namba T473 CJM lililokuwa likitoka Mugumu wilayani Serengeti kuelekea Mwanza ilitokea muda wa saa tano asubuhi eneo la njia panda ya Bunda mjini


Taarifa ya awali iliyotolewa na Kamishna Msaidizi wa Polisi Philip Kalanje imesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya basi hilo liitwalo Nata Raha kufeli breki zake.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment