Monday, 4 January 2016

WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI LA LUWINZO LILIKUWA LIKITOKA NJOMBE KUELEKEA DAR ES SALAAM


Basi la abiria aina ya Scania, mali ya kampuni ya Luwinzo lenye namba za usajili T 782 ACR linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es salaam limepata ajali asubuhi ya leo katika eneo la Kinegembasi kata ya Mbalamaziwa, wilayani Mufindi Mkoani Iringa na kusababisha vifo vya watu wanne.

Basi hilo lililokuwa likisafiri kutokea Njombe kuelekea Dar es Salaam liligongana na lori lenye namba za usajilli T 718 CRV aina ya IVECO.

Lori hilo lililokuwa likitokea Songea kwenda Dar lilikuwa limebeba makaa ya mawe.
 
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi (Hospitali ya Mafinga) ameuthibitishia mtandao huu kupokea miili ya watu wanne waliopoteza maisha na wengine 32 waliojeruhiwa.

Waliofariki dunia wametambuliwa kwa majina ya Rashid Kibalala (47) aliyekuwa kondakta wa basi hilo, Salim Chamgwila (28) aliyekuwa mkaguzi wa tiketi (inspekta) na maiti ambazo hazijatambulika. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment