Tuesday, 19 January 2016

WAKRISTO KUMUOMBA MUNGU APUNGUZE JOTO DAR ES SALAAM NA MAENEO YA PWANI

Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu, Dkt. Charles Gadi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maombi ya kuombea joto liweze kupungua.

Taasisi ya Kidini ya Good News for All Ministry inatarajia kufanya maombi ya kumuomba Mungu kupunguza joto kali linaloendelea kuongezeka katika maeneo ya Dar es Salaam, Pwani na Visiwa vya Zanzibar.

Akizungumzia maombi hayo, Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Dk Charles Gadi alisema wanatarajia kufanya maombi siku ya Jumatano, Januari, 20 katika eneo la Feri jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa sita mchana.

“Wastani wa joto ambalo kwa sasa lipo jijini Dar es Salaam, Tanga na Visiwa vya Zanzibar linakadiriwa kufikia nyuzi joto 35 ambazo kiafya inaweza kuwa na athari kwa binadamu na sasa tunataka kumuomba Mungu kuliondoa joto hili,” aliongeza.

Askofu Gadi alisisitiza kuwa joto hili linaweza kusababisha matatizo kwa wananchi na hivyo kuamua kuliombea kwa Mungu kusudi aliondoe kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hapo mbeleni kwani tayari baadhi ya watu wanaugua mapele na joto bahari linaongezeka kwa kasi kiasi cha kuweza kusababisha mafuriko.


Aidha, aliwamba wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika maombi hayo ili kuomba kwa pamoja ili Mungu asikie sauti zetu na kuweza kupunguza joto katika mikoa iliyoathirika.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment