Thursday, 21 January 2016

SERIKALI YAFUTA MFUMO WA GPA KATIKA ELIMU, YAREJESHA WA DIVISHENI


Serikali imeliagiza Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kufanya mapitio ya mfumo unaotumika sasa wa wastani wa alama za mtihani (GPA), ili kuangalia uwezekano wa  kurejea katika mfumo wa awali wa kupanga madaraja kwa mfumo wa divisheni.

Akitoa agizo hilo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.  Joyce Ndalichako amesema pamoja na serikali kutoa siku saba kwa baraza hilo kutoa sababu ya kuhama kutoka mfumo wa divisheni na kwenda katika mfumo wa GPA, bado baraza hilo limekuwa likitoa maelezo zaidi kuliko sababu za kuhamia mfumo huo.

Alisema hoja ya kuwa mfumo huo ulitokana na maagizo ya serikali haina nguvu kwa kuwa tayari baraza hilo ndilo linalotakiwa  kubeba dhamana ya madaraja ya ufaulu na kuongeza kuwa baraza hilo linatakiwa kuweka viwango vya ufaulu kwa kuzingatia azma ya nchi kuelekea katika uchumi wa kati.

“Wizara haiwezi kufikia azma yake ya kuelekea uchumi wa kati bila kuhakikisha viwango vya ufaulu vinawezesha nchi kutoa watalaamu wenye stadi na maarifa stahiki  badala ya kuwa na wahitimu wengi wenye vyeti lakini hawakidhi mahitaji katika soko la ajira,’’ alisema.


Wadau mbalimbali wa elimu wamekuwa wakiulalamikia mfumo wa GPA kwani unaruhusu wanafunzi ambao hawakufaulu vizuri kuendelea na masomo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment