Monday, 11 January 2016

RAIS DK MAGUFULI AMTEMBELEA HOSPITALINI WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDERICK SUMAYE

Rais Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na wazir mkuu mstaafu Mh.Fredrick Sumaye katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Rais DkJohn Pombe Magufuli leo amefika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye anayesumbuliwa na malazi ya Moyo.

Pamoja na kumpa pole, Rais Magufuli amemuombea apone haraka ili arudi kwenye majukumu yake ya kawaida.

Akizungumza baada ya ujio wa Rais Magufuli; Sumaye amesema kitendo cha Rais kumtembelea hospitalini hapo kinaonesha jinsi anavyojali na kuwapenda watu wake bila kujali itikadi zao za kisiasa.


Kuhusu afya yake Sumaye amesema hali yake inaendelea vizuri huku akitumaini kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo baada ya muda mfupi kutokana na huduma nzuri anazopata. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment