Wednesday, 13 January 2016

PATO LA TAIFA LAONGEZEKA

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu dkt. Albina Chuwa (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Serikali imeendelea kutoa huduma za kijamii zikiwemo umeme, afya na maji kwa ufanisi mkubwa kutokana na ongezeko la pato la Taifa katika kipindi cha robo mwaka wa 2015.

Akibainisha ongezeko hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa pato la Taifa limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ikilinganishwa na asilimia 5.4 katika kipindi cha mwaka 2014.

Dkt. Chuwa ameongeza kuwa ongezeko hilo limeweza kwenda sanjari na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa na huduma nje ya nchi kwa takribani asilimia 3.3 ambapo bidhaa na huduma zilizochangia ongezeko hilo ni pamoja na Dhahabu, Almasi, Madini Mengine na Utalii.


“Baadhi ya shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi kubwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2015 ni pamoja na Ujenzi asilimia 17.6, Uchukuzi na Uhifadhi asilimia 10.6, Uendeshaji Serikali na Ulinzi  asilimia 10.6 na Uchimbaji Madini na Kokoto asilimia 8.0,”alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment