Tuesday, 5 January 2016

NCHEMBA AKUNJUA MAKUCHA, ATUMBUA MAJIPU KWA KUWANG'OA WAKURUGENZI WA NARCO

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akikagua ujenzi wa ujenzi wa machinjio unao sua sua.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba ametangaza kuwasimamisha kazi wakurugenzi wote wa bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kufuatia upotevu wa Billion 5.7 zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa machinjio.

Akizungumza na Waandishi wa Habari  baada ya  kufanya ziara ya siku moja kukagua mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa ya ranchi ya Taifa ya Ruvu, Nchemba amesema ujenzi wa ranchi  ya Taifa ya Ruvu ulianza mwaka 2010 lakini hadi sasa haujakamilika kutokana na uzembe  na kukosa uzalendo kwa baadhi ya watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia mali  ya Umma.

Licha ya kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao amechukua maamuzi mengine ambayo ni Kumsimamisha kazi  mkurugenzi wa ranchi za Taifa kwa kushindwa kusimamia mradi huo ulioliingizia Taifa hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Ameagiza ndani ya siku 7 kupitia wataalam wa wizara wahakikishe wanampelekea ripoti ya thamani ya fedha inayohitajika kumalizia ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa.

Maaamuzi mengine ni kuagiaza  wahusika wote walioshiriki kuliingizia Taifa hasara hiyo wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria  kwa ajili ya hatua za kinidhamu.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment