Sunday, 17 January 2016

NAPE AANZA NA GAZETI LA MAWIO, ALIFUNGIA MILELE

wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nauye.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nauye ametangaza rasmi kulifungia  gazeti la kila wiki la MAWIO linalochapishwa na kampuni ya Victoria Media Services Ltd kwa muda wote kuanzia sasa.

Hatua hiyo inafuatia   tangazo lake lililotolewa kupitia gazeti la Serikali notisi namba 55 ya Januari 15, 2016; kaika notisi hiyo Serikali imebainisha kuwa imechukua uamuzi huo wa kulifungia gazeti la Mawio kwa muda wote kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo kupitia sheria ya magazeti ya mwaka 1976 sura ya 229 kifungu cha 25(1).

“Mawio linatakiwa kusimamisha uchapishaji wake kwa kipindi chote ikiwemo pia katika vyombo vya mawasiliano vya kielektroniki kuanzia Januari 15, 2016”, ilisema sehemu ya tangazo hilo ambalo limetolewa katika gazeti la serikali, likisainiwa na waziri Nape Nauye.

Hata hivyo tangazo hilo halifafanua ni makosa gani  yaliyosababisha serikali ichukue uamuzi wa kulifungia gazeti hilo.

Hivi karibuni serikali ililiandikia barua gazeti hilo na kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kutoa maelezo ya kwanini gazeti hilo lisifungiwe kufuatia makala zake mbili zenye vichwa vya habari “Hosea kortini” na “Seif Rais Zanzibar ambazo zilidaiwa kuzua taharuki.

kabla ya gazeti hilo kufungiwa lilikuwa likiendeshwa kupitia kampuni Hali Halisi Publishers ya Saed Kubenea ambayo pia inamiliki gazeti la kila wiki la MwanaHALISI ambalo pia liliwahi kufungiwa kwa zaidi ya miaka mitatu kabla ya kurejeshwa kwa amri ya Mahakama Kuu mwezi Agosti, 2015.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment