Tuesday, 19 January 2016

MSAJILI AIBANA CCM ZANZIBAR KWA UBAGUZI

Msajili wa vyama vya siasa Jaji Fransis Mutungi.

Chama cha Mapinduzi Visiwani Zanzibar kimezidi kubanwa kufuatia baadhi ya  wananchama wake kuweka ujumbe wenye maneno yenye ubaguzi wa Rangi wakati wa sherehe za Mapinduzi.

Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema amewaandikia barua  CCM  wajieleze  kuhusu ujumbe huo wa kibaguzi ulioonekana na kukemewa vikali na baadhi ya wanasiasa akiwemo Kiongozi mkuu chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe.

Kufuatia ujumbe huo Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) lilitangaza kumfikisha Mahakamani , Jaji Mutungi kwa kushindwa  kukifuta Chama Chama Mapinduzi kwa ujumbe huo wa Kibaguzi.

Akiwajibu Bavicha Mutungi amewataka   kabla ya  kumfikisha  Mahakamani  ni vyema kwanza wangemuuliza na kuwa na uhakika kwani tayari ameshachukua hatua za kisheria dhidi ya CCM.

“Wanatakiwa kuwa na uhakika kwanza, Mimi nimeshawachukulia hatua CCM, tena hatua kwa mujibu wa sheria. alisema Jaji Mutungi. 

Akizungumzia mgogoro wa kisiasa  Zanzibar Mutungi amesema tayari ofisi yake imeshaingilia mgogoro wa uchaguzi unaoendelea visiwani humo kwa kuwa unawahusu wadau ambao ni vyama vya siasa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment