Monday, 4 January 2016

MBUNGE WA KINONDONI ATINGA MAHAKAMANI KUZUIA BOMOABOMOA INAYOENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM

Bomoa bomoa katika Bonge la mto msimbazi.

SIKU moja kabla ya kuanza kwa zoezi la bomoabomoa jijini Dar es Salaam, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Maulid Mtulia amewasilisha mahakamani shauri la kupinga zoezi hilo.

Shauri hilo lenye uwakilishi wa wananchi nane limeanza kusikilizwa leo na litaendelea tena kesho katika mahakama Kuu kitengo cha Ardhi.

Akizungumzia kesi hiyo, Mtulia amesema shauri hilo lilifunguliwa mahakamani hapo Desemba 22 na kupata faili rasmi Desemba 28 mwaka jana.

Katika shauri hilo, walalamikaji wanaiomba mahakama kuamuru usitishwaji wa zoezi la bomoa bomoa ili kuwapa muda zaidi wa kujiandaa kuondoka katika maeneo hayo huku pia wakiomba mamlaka husika ziwatafutie makazi mbadala

Reactions:

0 comments:

Post a Comment