Sunday, 31 January 2016

MAJANGILI WA TEMBO WATUNGUA CHOPA, WAUA RUBANI NA TEMBO WATATU


Mtihani wa kwanza umemkumba Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni majangili  kuitungua kwa risasi helkopta ya doria ya wanyamapori katika pori la akiba la maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti na kumuua rubani wa helkopita pamoja na kumjeruhi askari mmoja wa wanyamapori.

Waziri huyo alifika katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji haramu wa maliasili kuanzia sasa.

Katika tukio hilo Rubani wa Chopa kepteni Roger Gower raia wa Uingereza alifariki dunia.

Maghembe  amesema kuwa kamwe tukio hilo haliwezi kuachwa lipite bila hatua madhubuti kuchukuliwa huku akiwaonya baadhi ya watumishi wa serikali na askari wa wanyamapori wanaoshirikiana na wahalifu kuwa sasa kiama chao kimefika.

Kwa upande wake kamanda wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea juzi jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria.

Katika tukio hilo lililopelekea watu watatu kushikiliwa na Polisi kwa mahojiano, tembo watatu waliuawa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment