Thursday, 14 January 2016

MAJALIWA: TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA RWANDA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura. Ambapo amemuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Rwanda.

Akizungumza na Balozi  Kayihura  jana ,(jumatano 13, 2016) ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amemshukuru  Balozi huyo kwa kumtembelea na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano ulipo baina ya nchi hizi mbili.

 “Nia yetu ni kushirikiana kwa pamoja kwa kuunganisha wafanyabiashara wetu, kwa kutumia Bandari  ya Dar es salaam na reli ya kati, ambayo tutajenga kwa  kiwango cha kisasa ‘standard gauge’  ili ziweze kubeba mizigo mingi na kwenda mwendo wa kasi” alisema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Balozi wa Rwanda, Kayihura amesema Tanzania na Rwanda ni nchi marafiki na zinafanyakazi wa pamoja, Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania kikanda na kimataifa.

“Tunatumia Bandari ya Dar es salaam na Mombasa, tunashukuru kwa namna ambavyo mnaboresha Bandari ya Dar es Salaam, kwani Rwanda inafaidika pia kwa vile mizigo yetu mingi karibu asilimia 75 husafirishwa  kupitia bandari hii”  alisema Balozi Kayihura.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
ALHAMISI, JANUARI 14, 2016.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment