Sunday, 3 January 2016

MAFURIKO YASITISHA SAFARI ZA TRENI

Treni mpya ya abiria yenye kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam na mikoa ya Kigoma na Mwanza, ikiwa kwenye kituo kikuu cha reli (TRL),Dares salaam.

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitisha kwa muda usiojulikana huduma zake baada ya eneo la reli ya kati ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma kukumbwa na Mafuriko.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana inaonesha eneo lililoathiriwa na mafuriko ni kubwa hali iliyoathiri safari hizo.

Katika kukabiliana na hali hiyo amesema wahandisi na mafundi wa TRL wako katika eneo la mafuriko ili kutathmini madhara na ukubwa kazi inayotakiwa kufanywa kama miundombinu ya reli hiyo imeharibika.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment