Monday, 11 January 2016

MAALIM SEIFA APINGA UCHAGUZI WA MARUDIO VISIWANI ZANZIBAR


KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia aliwania urais wa visiwa vya Zanzibar na kujitangaza mshindi kabla Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar haijafuta matokeo ya uchaguzi huo amekutana na wanahabari hii leo na kupinga mipango aliyoiita inatokana na shinikizo la baadhi ya viongozi wa CCM na wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya kurudia uchaguzi huo.

Maalim Seif Sharif Hamad amesema kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar ni ajenda inayokosa uhalali wa kikatiba na kisheria hivyo kutokuwa na uhalali wowote .

Alisema ili kuleta muafaka wa kisiasa katika visiwa hivyo na kukubali matakwa ya wananchi wake suluhisho pekee ni kwa tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi halali wa uchaguzi huo.

Alisema taarifa za awali kutoka kwa mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ya uchaguzi visiwani humo yanaonesha Maalimu Seif alipata kura zaidi ya 200,000 ambazo ni sawa na asilimia 52 huku Dk Mohamed Sheif wa CCM akipata kura zaidi ya 180,000 ambazo ni sawa na asilimia 46.

Maalim Seif amesema kazi ya kuyatangaza matokeo hayo apewe Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo badala ya Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jescha Salim Jecha anayetakiwa kuachia ngazi na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kwa kuharibu uchaguzi huo kwasababu zake binafsi na shinikizo la kisiasa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment