Thursday, 14 January 2016

LUKUVI ATOA SIKU 18 ZA KUVUNJA JENGO LA GHOROFA 16 DAR


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa siku 18 kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kuvunja jengo la ghorofa 16 lililopo katika Mtaa wa Indira Gandhi kabla halijaleta maafa.

Akizungumza katika jengo hilo, Lukuvi alisema anashangaa hadi sasa kazi ya kuvunja jengo hilo haijaanza licha ya manispaa kuelekezwa kulivunja.

Uamuzi wa Serikali  kulivunja ulikuja baada kuporomoka kwa jengo katika mtaa huo lililosababisha vifo vya watu 37 na wengine 18 kujeruhiwa mwaka 2013.

Lukuvi alisema kuanzia Februari Mosi uvunjaji wa jengo hilo unatakiwa kuanza vinginevyo wahusika wajiandae kuchukuliwa hatua.

“Nataka nikipita hapa siku yoyote kuanzia mwezi ujao nikute mkandarasi anabomoa jengo hili vinginevyo hatutaelewana,” alisema. Jengo hilo linamilikiwa kwa pamoja kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Ali Raza Investment

Reactions:

0 comments:

Post a Comment