Friday, 22 January 2016

JECHA ATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jesha Salum Jecha.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya Marudio ya Uchaguzi  wa Zanzibar uliofutwa mwaka jana kutokana na kile kilichoelezwa kwamba uligubikwa na kasoro kadhaa.

Mwenyekiti wa ZEC,  Jecha Salum Jecha ametangaza tarehe hiyo  ya Marudio ya Uchaguzi wa Zanzibar kuwa ni Machi 20, mwaka huu.


 Akizungumzia kuhusu wagombea watakaoshiriki katika uchaguzi huo Jecha amesema wagombea watakuwa walewale waliogombea kwa Nafasi ya Urais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani na kwamba hakuna chama wale mgombea atakayeruhusiwa kufanya kampeni.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment