Saturday, 9 January 2016

HII NDIO PICHA RASMI YA DK JOHN MAGUFULI KWA MATUMIZI YA OFISI MBALIMBALI ZA UMMA NA BINASFI

Watendaji wa Idara ya Habari Maelezo waki onesha Picha ya Rais Magufuli.

Serikali imetoa onyo kwa wale wote wanaosambaza  picha isiyo rasmi kwa matumizi ya ofisi ya Rais Dk John Magufuli wakati ikitangaza picha rasmi kwa matumizi hayo jana.

Kwa kupitia Idara ya Habari Maelezo, serikali ilitangaza rasmi picha ya Dk Magufuli iliyoanza kuuzwa jana Januari 08, 2015, katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Mtaa wa Samora.

Nakala ya picha inauzwa kwa Sh 15,000 bila fremu huku ile ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikiuzwa Sh 5,000 tu. 

Aidha, Picha hizo zitauzwa katika Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Picha hizo zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za Umma, Mashirika na Ofisi binafsi.  Kila ofisi inatakiwa iwe na picha ya Mhe. Rais pamoja na Baba wa Taifa.

Idara hiyo ya Habari(MAELEZO) imesema ndio yenye Haki miliki ya picha hiyo  itawachukulia hatua za kisheria  wataokutwa na picha tofauti na waliyo itoa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment