Sunday, 17 January 2016

HASHIM RUNGWE APINGA UCHAGUZI ZANZIBAR KURUDIWA NA MAZUNGUMZO BAINA YA CUF NA CCM


Aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CHAUMMA, Hashim Rungwe amesema kuwa  chama chake hakikubaliani na mazungumzo yeyote ya kutafuta suluhu ya Uchaguzi Mkuu Visiwani Zanzibar baina ya mgombea urais kupitia  CUF, Maalim Seif Sharrif Hammad na Dk Ali Mohamed Shein wa CCM.

Pamoja na kutokubaliana na azma ya kurudiwa kwa uchaguzi visiwani humo, Rungwe amesema mazungumzo hayo hayakubaliki kwasababu hayajashirikisha wagombea kutoka vyama vingine.

Katika uchaguzi huo uliofutwa, CHAUMMA kilimsimamisha  mgombea urais, Mohammed Masoud   ambaye pia amepinga vikali Mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha kufuta uchaguzi  huo na kuitaka tume hiyo kutumia uwezo wake kuzitatua changamoto na kasoro zilizojitokeza kabla ya kufikia hatua hiyo.


Rungwe pia amekemea na kulaani vitendo vya kibaguzi vilivyooneshwa katika sherehe za Mapinduzi Zanzibar siku ya tarehe 12, Januari.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment