Saturday, 23 January 2016

FIGISUFIGISU YAGUBIKA MASHINDANO YA MISS TANZANIA

Msemaji wa Kamati ya Kuratibu Miss Tanzania Joketi Mwegelo akitoa maelezo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) namna Kamati hiyo ilivyokuwa ikijitahidi kubadili mfumo ili kubadilisha muonekano wa mashindano ya urembo(Miss Tanzania) kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Juma Pinto.

Kamati ya kuratibu Miss Tanzania imejitoa rasmi kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kuanzia leo Januari 21 Mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Juma Pinto alisema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam.

“Tumekujakutoa taarifa kwamba, kama tulivyo teuliwa na kampuni ya Lino International Agency, kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano ya Miss Tanzania, kamati yangu imeamua kujitoa kutokana na majukumu ya kamati kuingiliwa na kampuni hiyo,” alisema Pinto.

Pinto aliongeza kwa kusema kuwa kamati yake ilipewa jukumu la kuendesha mashindano na kuwajibika kufanya kila kitu na Lino itakuwa kama washauri, lakini badala yake Lino imetaka kuhodhi majukumu yote na kamati ikawa ni ya kutafuta wadhamini.

Kamati hiyo imefanya vikao vingi vya kuhakikisha mashindano yanaboreshwa na kubadilisha mfumo ili kuifanya Miss Tanzania kuwa na mwonekano tofauti kama ambavyo Lino ilivyoamua kuweka kamati mpya ili kuboresha mashindano hayo.

Kutokana na kutopata muafaka katika vikao hivyo vya kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Kamati ya kuratibu mashindano hayo kwa nia njema na wala si kwa ubaya imeamua kujitoa katika Mashindano hayo.

Aidha, Pinto amewaomba radhi wadhamini ambao wameshaongea nao kama kamati na walioonesha nia ya kuwasaidia amewataka kuendelea kufanya mawasiliano na kampuni ya Lino kwani madhumuni ni kudhamini mashindano na sio kamati.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment