Saturday, 16 January 2016

DIWANI WA KATA YA IGOMBAVANU WILAYANI MUFINDI MKOANI IRINGA AFARIKI DUNIA


Diwani wa kata ya Igombavanu iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, HABIBU KILONGE kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) amefariki Dunia katika hospitali ya wilaya ya Mufindi usiku wa kuamkia leo alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Taarifa ya mwenyekiti wa Halmsahauri ya Wilaya ya Mufindi, Festo Mgina iliyotolewa kupitia kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri hiyo imeeleza kuwa, marehemu aligua kwa zaidi ya mwezi mmoja kabla hajafikwa na mauti.

Akizungumzia ratiba ya mazishi, Mgina amesema marehemu atazikwa Januari 17, Jumapili ijayo kijijini kwake Kichiwa, kata ya Mtwango mkoani Njombe.

Kabla ya mwili wake kusafirishwa kuelekea Njombe, mwili wa marehemu utapelekwa katika kata kata ya Igombavanu ambako utaagwa na wapiga kura wake..
Mgina alisema shughuli ya kuaga mwili wa marehemu itafanywa kati ya Saa 2.00 na Saa 5.00 asubuhi.

Marehemu Kilonge alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa diwani wa kata ya Igombavanu katika uchaguzi Mkuu uliyofanyika Oktoba mwaka jana.

Katika uchaguzi huo diwani huyo alipata kura 2,034 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kurika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyepata kura 361.

Mpaka mauti inamkuta diwani huyo likuwa amehudhuria kikao kimoja pekee, ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kuapishwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment