Thursday, 14 January 2016

CCM WAMPOZA MTOTO WA SOKOINE, WAMPA UJUMBE WA NEC MONDULI


Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, hayati Edward Sokoine, Namelock Sokoine amepita bila kupingwa katika nafasi ya mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Wilaya ya Monduli na kuziba nafasi hiyo iliachwa wazi na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa aliyehamia Chadema.

Lowassa alijiengua CCM na kujiunga na Chadema na kugombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita akiunga mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro alisema jana kuwa Namelock ambaye pia aligombea ubunge katika jimbo hilo na kushindwa na mgombea wa Chadema, Julius Kalanga, amepita bila kupingwa baada ya mpinzani wake Lanyoni ole Supuku kutorejesha fomu.


Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo iliyokuwa wazi baada ya Reuben Ole Koney kuhamia Chadema, imepata mrithi, Loata Sanare ambaye pia amepita bila kupingwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment